Fahamu Kuhusu Kodi ya Ardhi Nchini Tanzania

UTANGULIZI

Katika Makala hii tutajadili kiini cha kodi ya ardhi, uamuzi wa kiasi cha kodi, ukadiriaji pamoja na ulipaji wa Kodi ya Ardhi.


A: KIINI CHA KODI YA ARDHI NA UAMUZI WA KIASI CHA KODI

Ardhi yote nchini Tanzania ni mali ya umma na imekabidhiwa kwa Raisi kama mdhamini (msimamizi) mkuu kwa niaba ya watanzania wote. Hii inamaanisha kuwa ni Rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya umiliki wa ardhi (Hati y Hatima). Wananchi wote ni wapangaji katika ardhi na hivyo inapaswa kulipa Kodi ya ardhi.

Kiasi cha Kodi ya Ardhi  huamuliwa kwa kuangalia vitu vifuatavyo;

i) Ukubwa wa ardhi
ii) Matumizi ya ardhi
iii) Mahali ilipo ardhi


B: UKADIRIAJI WA KODI YA ARDHI

Kuna njia mbalimbali za kufahamu kiasi cha kodi ya ardhi unachopaswa kulipa kwa mwaka husika. Njia hizo ni;
a) Kupitia simu ya mkononi
b) Mfumo wa Kukadiria Kodi ya Ardhi kwa Njia ya Mtandao (Online Self Assessment
c) Mfumo wa Taarifa za Ulipaji Kodi za Ardhi (LRMS)

a) Kupitia Simu ya Mkononi


Njia ya Kwanza

i) Bonyeza *152*00#

ii) Chagua namba 4 (Malipo ya Serikali)

iii) Chagua namba 2 (Kadiria kodi ya kiwanja)

iv) Chagua namba 1 (Dar) or number 2 (Mikoa mingine)

v) Kadiria kodi ya ardhi kwa kutumia Namba ya Hati (chagua namba 1) au kwa kutumia ID ya Kiwanja (Lot ID) (chagua namba 2).

vi) Ingiza namba uliyochagua kutumia katika hatua ya v) hapo juu (Namba ya Hati au ID ya Kiwanja)

vii) Thibitisha ombi la kukadiria kodi ya kiwanja kilichopo (chagua 1)

viii) Subiri ujumbe mfupi wenye namba ya kulipia (Control Number). Utatumia namba hii kufanya malipo.



Njia ya Pili

i) Katika sehemu ya kuandikia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), andika neno Hati ikifuatiwa na namba ya hati, kisha andika namba 2;
    Kwa mfano:  Hati 12345 2
                   Au
   Andika neno ID ikifuatiwa na   namba ya ID (Lot ID), kisha andika namba 2;
   Kwa mfano: ID 12345 2

ii) Kisha tuma kwenda namba 15200

iii) Subiri ujumbe mfupi wenye namba ya kulipia (Control Number). Utatumia namba hii kufanya malipo.


b) Mfumo wa Taarifa za Ulipaji Kodi za Ardhi (LRMS)

Hii huhusisha kutembelea ofisi za ardhi za eneo ulilopo kisha kodi itakadiriwa kwa kutumia Mfumo wa Taarifa za Ulipaji Kodi za Ardhi (LRMS).
Unashauriwa kutembelea ofisi za ardhi kwa taarifa na msaada zaidi.

c) Mfumo wa Kukadiria Kodi ya Ardhi kwa Njia ya Mtandao (Online Self Assessment)


Ukadiriaji wa kodi ya ardhi hufanyika kwa kutembelea tovuti hii:
Hapo utajaza taarifa zinazohitajika na kisha utasubiria mrejesho.
Mwonekano wa tovuti unaoneshwa hapa chini;


C: MALIPO YA KODI YA ARDHI


Kodi ya Ardhi hulipwa mara moja kwa mwaka, kabla ya tarehe 30, Juni kila mwaka. Pia, Kodi ya Ardhi hulipwa kwa kutumia huduma za kifedha za simu ya mkononi kama vile Tigopesa na  M-Pesa au huduma za kibenki kama vile NMB na CRDB.

HITIMISHO

Tunatumai kuwa sasa umejifunza kitu kikubwa kuhusu Kodi ya Ardhi. Ukiwa kama raia muwajibikaji unashauriwa kulipa Kodi ya Ardhi kwa wakati. Kwa kufanya hivyo, sio tu utaepuka hatua za kisheria, bali pia utasaidia kuongeza mapato ya serikali.
The Aliland inapenda kukushauri kutembelea ofisi za ardhi za eneo ulilopo ili kupata muongozo mzuri wa mambo yanayohusiana na kodi ya ardhi, hasa kipengele cha malipo.

Comments

alpha said…
Mifumo your haifanyi kazi labda kqenda ofisi za Ardhi.
Mwaka Jana Mimi nikilipa kupigia hiyo mifumo lkn mwaka hui sijuhi mini kimetokea.
Moderator 1 said…
Habari Alpha.
Ahsante kwa mchango wako. Huenda ni changamoto za kimfumo zimetokea. Unashauriwa kwenda ofisi ya Ardhi iliyo karibu nawe.
Anonymous said…
Samahani mm nlinunua kiwanja kwa mtu nika jenga sasa nataka kupata hati je natakiwa nilipe ada ambazo mmiliki wa kiwanja alive pita au natakiwa nilipe tangu nmeanza kumiliki?
Anonymous said…
Vizuri kwa kuelimisha lakini ujatueleza ni namna gani ya kujua kiasi sahihi kulingana na ukubwa wa eneo na sehemu lilipo