Fahamu Kuhusu Kodi ya Ardhi Nchini Tanzania
UTANGULIZI
Katika Makala hii
tutajadili kiini cha kodi ya ardhi, uamuzi wa kiasi cha kodi, ukadiriaji pamoja
na ulipaji wa Kodi ya Ardhi.
A: KIINI CHA KODI YA ARDHI NA UAMUZI WA KIASI CHA KODI
Ardhi yote nchini
Tanzania ni mali ya umma na imekabidhiwa kwa Raisi kama mdhamini (msimamizi)
mkuu kwa niaba ya watanzania wote. Hii inamaanisha kuwa ni Rais pekee ndiye
mwenye mamlaka ya mwisho ya umiliki wa ardhi (Hati y Hatima). Wananchi wote ni
wapangaji katika ardhi na hivyo inapaswa kulipa Kodi ya ardhi.
Kiasi cha Kodi ya Ardhi huamuliwa kwa
kuangalia vitu vifuatavyo;
i) Ukubwa wa
ardhi
ii) Matumizi
ya ardhi
iii) Mahali
ilipo ardhi
B: UKADIRIAJI WA KODI YA ARDHI
Kuna njia mbalimbali
za kufahamu kiasi cha kodi ya ardhi unachopaswa kulipa kwa mwaka husika. Njia
hizo ni;
a) Kupitia
simu ya mkononi
b) Mfumo wa Kukadiria Kodi ya
Ardhi kwa Njia ya Mtandao (Online
Self Assessment
c) Mfumo wa
Taarifa za Ulipaji Kodi za Ardhi (LRMS)
a) Kupitia Simu ya Mkononi
Njia ya Kwanza
i) Bonyeza *152*00#
ii) Chagua namba 4 (Malipo ya Serikali)
iii) Chagua namba 2 (Kadiria kodi ya kiwanja)
iv) Chagua namba 1 (Dar) or number 2 (Mikoa mingine)
v) Kadiria kodi ya ardhi kwa kutumia Namba ya Hati (chagua namba 1) au kwa kutumia ID ya Kiwanja (Lot ID) (chagua namba 2).
vi) Ingiza namba uliyochagua kutumia katika hatua ya v) hapo juu (Namba ya Hati au ID ya Kiwanja)
vii) Thibitisha ombi la kukadiria kodi ya kiwanja kilichopo (chagua 1)
viii) Subiri ujumbe mfupi wenye namba ya kulipia (Control Number). Utatumia namba hii kufanya malipo.
i) Bonyeza *152*00#
ii) Chagua namba 4 (Malipo ya Serikali)
iii) Chagua namba 2 (Kadiria kodi ya kiwanja)
iv) Chagua namba 1 (Dar) or number 2 (Mikoa mingine)
v) Kadiria kodi ya ardhi kwa kutumia Namba ya Hati (chagua namba 1) au kwa kutumia ID ya Kiwanja (Lot ID) (chagua namba 2).
vi) Ingiza namba uliyochagua kutumia katika hatua ya v) hapo juu (Namba ya Hati au ID ya Kiwanja)
vii) Thibitisha ombi la kukadiria kodi ya kiwanja kilichopo (chagua 1)
viii) Subiri ujumbe mfupi wenye namba ya kulipia (Control Number). Utatumia namba hii kufanya malipo.
Njia ya Pili
i) Katika sehemu ya kuandikia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), andika
neno Hati ikifuatiwa na namba ya hati, kisha andika namba 2;
Kwa mfano: Hati 12345 2
Au
Andika neno ID ikifuatiwa
na namba ya ID (Lot ID), kisha
andika namba 2;
Kwa mfano: ID 12345 2
ii) Kisha tuma kwenda
namba 15200
iii) Subiri ujumbe
mfupi wenye namba ya kulipia (Control Number). Utatumia namba hii kufanya
malipo.
b) Mfumo wa Taarifa za Ulipaji Kodi za Ardhi (LRMS)
Hii huhusisha
kutembelea ofisi za ardhi za eneo ulilopo kisha kodi itakadiriwa kwa kutumia
Mfumo wa Taarifa za Ulipaji Kodi za Ardhi (LRMS).
Unashauriwa kutembelea
ofisi za ardhi kwa taarifa na msaada zaidi.
c) Mfumo wa Kukadiria Kodi ya Ardhi kwa Njia ya Mtandao (Online Self Assessment)
Ukadiriaji wa kodi ya ardhi hufanyika kwa
kutembelea tovuti hii:
Hapo utajaza taarifa zinazohitajika na
kisha utasubiria mrejesho.
Mwonekano wa tovuti unaoneshwa hapa chini;
C: MALIPO YA KODI YA ARDHI
Kodi ya Ardhi hulipwa mara moja kwa mwaka,
kabla ya tarehe 30, Juni kila mwaka. Pia, Kodi ya Ardhi hulipwa kwa kutumia
huduma za kifedha za simu ya mkononi kama vile Tigopesa na M-Pesa au huduma za kibenki kama vile NMB na
CRDB.
HITIMISHO
Tunatumai kuwa sasa umejifunza kitu kikubwa
kuhusu Kodi ya Ardhi. Ukiwa kama raia muwajibikaji unashauriwa kulipa Kodi ya
Ardhi kwa wakati. Kwa kufanya hivyo, sio tu utaepuka hatua za kisheria, bali
pia utasaidia kuongeza mapato ya serikali.
The Aliland inapenda kukushauri
kutembelea ofisi za ardhi za eneo ulilopo ili kupata muongozo mzuri wa mambo
yanayohusiana na kodi ya ardhi, hasa kipengele cha malipo.
Comments
Mwaka Jana Mimi nikilipa kupigia hiyo mifumo lkn mwaka hui sijuhi mini kimetokea.
Ahsante kwa mchango wako. Huenda ni changamoto za kimfumo zimetokea. Unashauriwa kwenda ofisi ya Ardhi iliyo karibu nawe.