MAKALA 004S: Mahitaji na Hatua za Kufuata ili Kupata Hati ya Umiliki
READ THIS ARTICLE IN ENGLISH
UTANGULIZI
Katika makala hii, mahitaji na hatua muhimu zinazohusika katika kupata Hati ya Umiliki ya Kiserikali zinaelezewa.
A: MAHITAJI ILI KUPATA HATI YA UMILIKI
b) Uthibitisho wa umiliki wa ardhi.
c) Uthibitisho wa utaifa.
d) Picha za pasipoti.
e) Malipo ya gharama zinazohusiana na Hati ya Umiliki.
Hayo ni
mahitaji ya msingi,
Kamishna wa Ardhi anaweza kuhitaji taarifa au
mahitaji mengine ya ziada.
a) Ardhi Lazima Iwe Imepangwa na
Kupimwa
Hili ni sharti la msingi ambalo likiachwa litasababisha kutoendelea kwa
hatua zingine za
kupata Hati ya Umiliki. Upangaji na upimaji wa
ardhi unaweza kufanywa na mmoja kati ya hawa wafuatao;
i)Serikali
Hapa wahusika ni idara ya upimaji na ramani, na upangaji
katika mamlaka
husika kama vile Halmashauri ya Manispaa au Wilaya.
ii) Kampuni binafsi za upangaji na upimaji
Ni lazima mipango ya matumizi ya
ardhi na ramani zilizoandaliwa na kampuni binafsi zithibitishwe na mamlaka ya upangaji, na upimaji na ramani
katika Halmashauri
husika ya Manispaa au Wilaya.
b) Uthibitisho wa Uraia
Ni lazima muombaji wa
Hati ya Umiliki awe na kitambulisho kinathibitisha uraia
wake.
Kitambulisho hicho kinaweza kuwa Kitambulisho cha Taifa,
Hati ya Kusafiria, kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa, Leseni ya Udereva, na Kitambulisho cha Mpiga Kura.
Nyakati hizi
Kitambulisho cha Taifa kinasisitizwa
zaidi kuliko aina
zingine za vitambulisho.
Unakumbuka ustahiki wa
umiliki ardhi nchini Tanzania katika Makala 003S? Uthibitisho wa uraia unahitajika ili kuthibitisha kama
muombaji anastahiki
kumiliki ardhi kisheria.
c) Uthibitisho wa Umiliki wa Ardhi
Ni lazima muombaji apeleke nyaraka halali. zinazothibitisha
umiliki wa ardhi husika. Nyaraka hizo ni
kama vile Mkataba wa Mauziano (ya
ardhi), historia ya kiwanja, na nyaraka za
urithi.
e) Malipo ya Gharama Zinazohusiana na Hati ya Umiliki
Kupata
Hati ya Umiliki kunahusisha
gharama mbalimbali. Gharama hizi zinatambulika
kisheria, na zinaorodheshwa hapa
chini;
- Ada
ya Hati
-Ada
ya Usajili wa
Ardhi
-Kodi ya
Ardhi
-Tozo la Mbele
-Ada
ya Ramani ya
Hati
-Ushuru wa
Serikali
-Ada
ya Upimaji
Mjadala wa kina kuhusu
gharama zinazohusiana na
Hati ya Umiliki unapatikana
katika
Makala 005S.
B: HATUA ZA KUFUATA ILI KUPATA UMILIKI WA ARDHI KWA HATI
a) Kuwasilisha ombi la
umiliki
b) Uamuzi wa kugawiwa ardhi
c) Kupewa umiliki wa hati
a) Kuwasilisha Ombi la Umiliki
Maombi ya umiliki wa ardhi hufanyika kwa kujaza fomu ya maombi. Hii
ni fomu maalumu inayoitwa “Fomu
ya Ardhi Na. 19
(Maombi
ya Haki ya Kumiliki Ardhi).”
Fomu hii inapatikana
katika ofisi za
ardhi kwenye
Halmashauri ya Wilaya au Manispaa.
Baada ya kujaza fomu kwa ukamilifu, muombaji ataiwasilisha fomu hiyo
kwenye ofisi ya
ardhi kwa taratibu nyingine za kiofisi.
Kumbuka kuwa
fomu ya maombi itaambatanishwa na
mahitaji yaliyotajwa mwanzoni mwa
makala hii kadri utakavyopewa maelekezo kutoka ofisi ya
ardhi.
b) Uamuzi wa Kugawiwa Ardhi
Katika
hatua hii Kamishna wa Ardhi atafanya uamuzi wa kukubali au kukataa maombi ya
Hakimiliki. Endapo ataamua kunyima
umiliki wa ardhi,
atatakiwa kutoa
sababu za kufanya hivyo.
c) Kupata Umiliki wa Hati
Hati
ya Umiliki itatolewa iwapo
Kamishna ataridhika kuwa
muombaji wa hati ametimiza
masharti, na amefanya uamuzi wa
kutoa Hakimiliki.
Je, una swali lolote kuhusu makala hii?
Je, una nyongeza kuhusu kupata Hati ya Umiliki?
Usisite kutuandikia kwenye sehemu ya maoni.
Je, una swali lolote kuhusu makala hii?
Je, una nyongeza kuhusu kupata Hati ya Umiliki?
Usisite kutuandikia kwenye sehemu ya maoni.
Ahsante na Karibu!
The Aliland Team
Comments