KILA KITU UNACHOHITAJI KUFAHAMU KUHUSU MKUTANO MKUU WA NNE WA MWAKA WA WATHAMINI (VRB AGM) 2023
Mkutano Mkuu wa Nne wa Mwaka wa Wathamini ulifanyika tarehe 9 na 10 Novemba 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma.
Mkutano huu uliitishwa na Bodi ya Usajili wa Wathamini Tanzania (Valuers Registration Board - VRB).
Ipi Ilikuwa Mada Kuu ya Mkutano?
"Utafiti na Uchimbaji Madini kwa Maendeleo Endelevu ya Taifa: Tathmini ya Athari Haki-ardhi, Thamani na Fidia ya Ardhi"
Umeona Kiswahili chake ni kigumu, huh?
Kwa kiingereza mada inamaanisha "Harnessing Mineral Wealth for National Sustainable Development: Implication for Land Rights, Values and Compensation"
Nani Alihudhuria?
Wathamini, na Wadau wa Uthamini nchini Tanzania.
Mgeni Rasmi alikuwa nani?
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.
Mambo Yaliyojadiliwa
UADILIFU KATIKA UTHAMINI
Mgeni Rasmi alisisitiza kuhusu uadilifu miongoni mwa wathamini
"Kazi yenu (ya uthamini) inahitaji watumishi wenye weledi, wanaojituma wanaowajibika na waadilifu. Kazi ya uthamini sio kazi inayoruhusu watu wasiokuwa na maadili."
"Endeleeni kufanya kazi yenu muhimu kwa weledi, uaminifu na uadilifu (katika uthamini)."
Pia aliongezea kuwa,
"Kila mthamini anapaswa kujitathmini na kuona kama kazi zake za kila siku anafanya kwa wito. Nina imani mnaendelea kuthamini kazi yenu na kuheshimu taaluma yenu."
Video hapa chini inaonesha mambo yote aliyozungumza Mgeni Rasmi:
TATHMINI YA ATHARI HAKI-ARDHI, THAMANI NA FIDIA YA ARDHI
Hii ndio ilikuwa mada kuu ya Mkutano huu. Wathamini na wadau wa uthamini walijadili ni kwa namna gani utwaaji ardhi unavyokuwa na athari kwa mtu wa mwishi (mwathirika wa mradi wa utwaaji ardhi) na kwa kuzingatia haki-ardhi (land rights). Waliangazia zaidi katika miradi ya uchimbaji madini.
PRV Amani Kimola amezungumzia kwa kifupi kuhusu lengo kwenye video ifuatayo:
.......
FRV Robert Mwakasisye alipendekeza kuwa,"Uthamini wa fidia ni suala la katiba, kwani linagusa moja ya haki za msingi za umiliki wa mali. Hivyo tunapofanya tathmini kama hizo, tunapaswa kufanya chini ya wigo wa sheria. Hii itasaidia kusawazisha maslahi ya umma na ya waathirika wa miradi ya utwaaji ardhi (PAPs).."
.......
Kutokana na fidia kuendelea kutowatosheleza waathirika ya miradi ya utwaaji ardhi, FRV Elitruda Makupa alitoa mapendekezo kadhaa katika wasilisho lake, yakiwemo;
- Kuongeza uwezo wa Tanzania katika kusimamia sekta ya madini kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania ili kuimarisha haki za umiliki kwa wenye ardhi pamoja na fidia ya kutosha na ya haki.
- Kunahitajika mapitio ya sheria ya fidia. Ni miaka 56 imepita tangu Sheria ya Utwaaji Ardhi ya 1967 itungwe. Sheria hii mara chache hugusa upeo wote wa hasara zinazopatikana kwa waathirika wa miradi ya utwaaji ardhi (PAPs).
- Matumizi ya mwongozo wa Benki ya Dunia. Hii inaweza kusaidia kuboresha utaratibu wa kutathmini hasara na kutoa fidia inayostahili kwa wahusika.
1. Kuwe na kiwango cha chini cha ulipaji wa fidia.
FRV Anne Urassa
VIDEO ZAIDIHITIMISHO
Tunaipongeza Bodi ya Usajili wa Wathamini (VRB) kwa kuitisha mkutano huu na ilikuwa ni fursa muhimu kwa wadau wa tasnia ya uthamini. Baadhi ya faida za mkutano huo kwa wathamini ni pamoja na kuunganisha pamoja wataalamu wa uthamini, kuongeza maarifa, kujadiliana mambo ya kitaaluma na kuboresha ubora wa taaluma yetu.
Aliland Team
Comments