Posts

Showing posts from November, 2023

KILA KITU UNACHOHITAJI KUFAHAMU KUHUSU MKUTANO MKUU WA NNE WA MWAKA WA WATHAMINI (VRB AGM) 2023

Image
Mkutano Mkuu wa Nne wa Mwaka wa Wathamini ulifanyika tarehe 9 na 10 Novemba 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma. Mkutano huu uliitishwa na Bodi ya Usajili wa Wathamini Tanzania (Valuers Registration Board - VRB). Ipi Ilikuwa Mada Kuu ya Mkutano? "Utafiti na Uchimbaji Madini kwa Maendeleo Endelevu ya Taifa: Tathmini ya Athari Haki-ardhi, Thamani na Fidia ya Ardhi" Umeona Kiswahili chake ni kigumu, huh? Kwa kiingereza mada inamaanisha  "Harnessing Mineral Wealth for National Sustainable Development: Implication for Land Rights, Values and Compensation" Nani Alihudhuria? Wathamini, na Wadau wa Uthamini nchini Tanzania. Mgeni Rasmi alikuwa nani? Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa. Mambo Yaliyojadiliwa UADILIFU KATIKA UTHAMINI Mgeni Rasmi alisisitiza kuhusu uadilifu miongoni mwa wathamini "Kazi yenu (ya uthamini) inahitaji watumishi wenye weledi, wanaojituma wanaowajibika na waadilifu...